Polisi imeendesha msako wa raia wasiekuwa na vibali katika tarafa ya Buyenzi kwa kuwaelekeza kwenye uwanja wa mpira wa AFB kulikoendeshwa harakati hiyo, wageni waliekutwa kueshi kinyume cha sheria wamerejeshwa nchini kwao na wazalendo waliokosa vitambulisho walitozwa adabu ya pesa elfu 2 sarafu za Burundi.
Yote hayo ni katika dhamira ya kufahamu vema wanaomiliki vibali bandia waweze kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria, kwa kuwatenganisha wageni na wazalendo kwa ushirikiano wa polisi na wakuu wa vitongoji katika tarafa ya Buyenzi.
Kwa ujumla wa watu 240 waliekamatwa, 200 hawakuwa na vitambulisho vya uraia na wale waliekutwa wakikamilika waliachwa huru .
Wakati wa harakati hiyo polisi ilimtia kizimbani mtu 1 aliekuwa akimiliki silaha pamoja na vifaa vingine vya kijeshi,akiwa alibaini kuwa vyote hivyo si vyake bali aliwekeshwa,uchunguzi umeanzishwa na polisi kutambuwa ukweli wa mambo.
Monday, 26 January 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment